Skip to main content

Baraza la haki za binadamu limejadili ulinzi kwa waandishi habari kwenye migogoro

Baraza la haki za binadamu limejadili ulinzi kwa waandishi habari kwenye migogoro

Akizungumza katika mkutano wa baraza la haki za binadamu ambao leo umejadili ulinzi kwa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro, mwakilishi maalumu wa kuchagiza na kulinda haki na uhuru wa mawazo na kujieleza amesema vyombo vya habari ni muhimu.

Ameongeza kuwa katika maeneo yenye migogoro waandishi wa habari na vyombo vya habari kwa ujumla vinakuwa na jukumu muhimu la kuweka bayana ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu wa vita.

Lakini pia ni jukumu lao kufuatilia hali hiyo na kushawishi umma kubadili mtazamo kuhusu vita ambavyo mara nyingi vinawafanya kuwa walengwa wa mashambulizi ya kimataifa.

(HUMANRIGHTS CLIP)