Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malipo ya uzeeni ni muhimu ili kujikwamua na umasikini:UM

Malipo ya uzeeni ni muhimu ili kujikwamua na umasikini:UM

Wataalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kwamba ni muhimu kwa serikali kuchukua hatua za kuwalinda vikongwe katika jamii kwa kuwapa malipo ya uzeeni ili kuwalinda dhidi ya umasikini.

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na umasikini Magdalena Sepulveda amesema jamii zinaacha utamaduni wa kuwasaidia vikongwe na hivyo wengi wao wanabaki bila msaada wowote.

Akizindua repoti yake kwa baraza la haki za binadamu mjini Geneva Bi Sepulveda amesema malipo ya uzeeni ni muhimu kulinda haki za wazee katika jamii.