Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA imeshitushwa na shambulio la Israel dhidi ya boti ya flotilla Gaza

UNRWA imeshitushwa na shambulio la Israel dhidi ya boti ya flotilla Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina (UNRWA) limesema limeshtushwa na kitendo cha majeshi ya Israel kushambulia boti ya flotilla iliyokuwa ikielekea Gaza na misaada ya kibinadamu.

Mwakilishi wa UNRWA mjini Brussels, Mathias Buchard, amesema wakati sio suala la shirika hilo kuamua nini kilichotokea kwa boti ya flotilla , boti hiyo ilikuwa njiani kujaribu kuvunja vizuizi vya Israel Gaza na kupeleka misaada ya kibinadamu inayohitajika eneo hilo.

Mathias Buchard amesema ni muhimu kuelewa kwamba hili sio jambo la kujaribu kubishana endapo hili ni suala la kibianadamu au la. Ametaja kwamba maafisa wa Israel wanasema hakuna mtafaruku lakini kuna ushahidi unaoonyesha mtafaruku upo kutokana na tathimini ya wajumbe na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Gaza.