Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama la UM lataka ufanyike uchunguzi wa kina dhidi ya shambulio la boti Gaza

Baraza la usalama la UM lataka ufanyike uchunguzi wa kina dhidi ya shambulio la boti Gaza

Mapema leo asubuhi baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa ya kulaani vikali operesheni za Israel dhidi ya boti za misaada za Gaza zinazosababisha vifo kwa raia .

Baraza hilo limetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina, usio na upendeleo na ulio wazi dhidi ya tukio la boti ya flotilla na limetaka boti zinazoshikiliwa na Israel kuachiliwa mara moja ikiwa ni pamoja na raia waliko katika boti hizo.

Taarifa hiyo ya baraza la usalama imetolewa na Rais mpya wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Juni balozi Claude Heller wa kutoka nchini Mexico.

(SAUTI  HELLER)

"Anasema baraza la usalama limeomba kuachiliwa mara moja kwa boti pamoja na raia wanaoshikiliwa na Israel. Baraza limeitaka Israel kuruhusu balozi kuweza kuingia, kuruhusu nchi husika kuchukua maiti zao na majeruhi mara moja, na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafika inakotakiwa."