Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICC imeipeleka Sudan kwenye baraza la usalama la UM

Mahakama ya ICC imeipeleka Sudan kwenye baraza la usalama la UM

Mahakama ya kimataifa ya uhalivu wa kivita, ICC imeipeleka Sudan kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baada ya nchi hiyo kushindwa kutoa ushirikiano unaotakiwa kuwafikisha mahakamani washukiwa wawili.

Washukiwa hao ni waziri wa zamani na kiongozi wa kundi la waasi lililojihami kwa silaha ambalo linaunga mkono na serikali. Watu hao wanashitakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita kwenye jimbo la Darfur, yakiwemo kuuawa raia na ubakaji wa wanawake.

Taarifa ya ICC inasema sasa ni wajibu wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ambayo linaona ni madhubuti. Makosa ya kivita yanayowakabili yanadaiwa kutekelezwa wakati wa mapigano kati ya serikali na wapiganaji wa Sudan People's Armed Forces, kundi la Janjaweed dhidi ya waasi wa Sudanese Liberation Army, SPLM na kundi la Justice and Equality Movement, JEM.