Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi wa Colombia bado wanajihusisha na ukiukaji wa haki za binadamu

Wanajeshi wa Colombia bado wanajihusisha na ukiukaji wa haki za binadamu

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia haki za Binadamu wamesema Colombia ambayo imekumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na ukiukaji wa haki za binadamu imechukua hatua ya kupunguza mauwaji,lakini bado wanajeshi wa nchi hiyo wanakisiwa kuhusika na mauwaji mengi nchini humo.

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Philip Alston katika ripoti yake baada ya uchunguzi kuanzia Juni mwaka jana amesema japo mauwaji hayo si sera ya serikali yamekuwa yakitekelezwa na baadhi ya vitengo vya wanajeshi mara kwa mara nchini humo.

Aliston amesema kwa kawaida watu hao wanaouawa huhadaiwa na kupelekwa katika maeneo ya mbali na kisha kuuawa na kuripoti kuwa waliuwawa katika mapambano na kisha baadae kutoa taarifa zisizokuwa za ukweli.