Siku ya Afrika inayoadhimishwa leo ina umuhimu gani kwa bara hilo na watu wake?

25 Mei 2010

Leo Mai 25 ni siku iliyotengwa rasmi na Umoja wa Afrika(AU)kuadhimisha siku ya Afrika. Je siku hii ina maana gani? nini umuhimu wake kwa bara la Afrika linalokabiliwa na matatizo kibao ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii?

Kuyachambua hayo naungana na Dr salim Ahmed Salim aliyeahi kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Nchi huru za Afrika wakati huo OAU na baadaye kubadilishwa jina na kuwa Umoja wa Afrika AU.

Dr Salim alishikilia wadhifa huo tangu Septemba 1989 hadi september 2001 na kuandika historia ya kushikilia madara hayo kwa muda mrefu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote.

Tuandamane

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter