Naibu Katibu Mkuu wa UM yuko Baku kwenye mkutano wa usawa wa kijinsia

Naibu Katibu Mkuu wa UM yuko Baku kwenye mkutano wa usawa wa kijinsia

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro yuko mjini Baku Azabaijan kuhudhuria mkutano wa usawa baiana ya wanaume na wanawake.

Akizungumza katika mkutano huo amesema hii fursa nzuri kwani mwaka huu ni 15 tangu mkutano wa kimataifa wa Beijing, ambao uliweka mikakati ya ukombozi wa mwanamke, pili Umoja wa Mataifa utakuwa na mkutano muhimu mwezi septemba kutathimini malengo ya milenia na moja wapo ni usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.

Lakini amesema mwezi Oktoba jumuiya ya kimataifa itaadhimisha miaka 10 ya azimio la baraza la usalama namba 1325 linalozungumzia wanawake, amani na usalama. Amesema matukio yote haya na mkutano wa Baku ni fursa nzuri kutathimini hatua zilizopigwa kuchagiza kisiasa na kuweza kuwa na miakakti madhubuti ili kuziba pengo lililopo baiana ya wanaume na wanawake duniani.