Skip to main content

UNICEF inahitaji fedha kuwasaidia watoto Jamhuri ya Afrika ya Kati

UNICEF inahitaji fedha kuwasaidia watoto Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto, UNICEF, linahitaji jumla ya dola milioni 4.2 ilikuwasaidia watoto walioathirika na ukosefu wa usalam na mapigano ya jadi katika Jmahuri ya Afrika ya Kati ambao wanamahitaji ya dharura.

Mpaigano ya muda mrefu pamoja na ukosefu wa usalama vinazidi kuaathiri maisha ya maelfu ya watoto Kaskazini na Mashariki mwa nchi hiyo. Karibu watu robo milioni wameathiriwa na mapigano nchini Jamhuri ya afrika ya Kati.

Baadhi ya changamoto ni kuzuka kwa magonjwa , ongezeko la bei ya chakula na bidhaa zingine muhimu na uhaba wa raslimali za kuwafikia watu katika baadhi ya maeneo mengine nchini.