Skip to main content

UNHCR yasihi wakimbizi wa Kisomali wasirejeshwe nyumbani kwa nguvu

UNHCR yasihi wakimbizi wa Kisomali wasirejeshwe nyumbani kwa nguvu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesihi mataifa yasiwaregeshe wakimbizii wanaotoka Somalia .

Ombi hilo limemetolewa baada ya wakimbizi 100 ya Wakisomali kurejeshwa nyumbani kwa nguvu na Saudi Arabia kati kati ya mwezi huu. UNHCR imesema kuwa kurejeshwa kwa wakimbizi kutoka katika eneo la katikati na Kusini mwa nchi hiyo iwe ni kwa hairi tu.

Msemaji wa UNHCR Melissa Fleming ametaja kuwa mataifa yana viwango tofauti kuhusiana na tathmini ya ulinzi kwa wakimbizi. Wakati huo huo Flemming amesema anatiwa wasi wasi na hali mbaya ya wakimbizi wa Kisomali duniani lakini ameongeza kuwa kuna haja ya kurekebisha viwango vya ulinzi wa wakimbizi duniani.