Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bank ya dunia yasema rushwa ya utegeaji imemea mizizi Afrika

Bank ya dunia yasema rushwa ya utegeaji imemea mizizi Afrika

Bank ya dunia imezitaka nchi za mataifa ynayoendele kukabiliana na tatizo la utegeaji kwa maendeleo ya mataifa yao.

Katika ripoti ya hivi karibuni Bank ya dunia inasema rusdhwa ya kimyakimya ambayo ni utegeaji inachangia pakubwa kurudisha nyumba maendeleo hususani kwa nchi masikini kama za Afrika.

Sekta kama za elimu na afya zimeonekana kuwa mbele katika kujihusisha na rushwa hiyo na sasa serikali zinatakiwa kujifunga kibwebwe kukabiliana nayo, la sivyo maendeleo yanayohitajika hayatopatikana. Pia malengo ya milenia yatakuwa hatarini.

Ni kwa nini tabia hiyoi imemea mizizi? ungana na mwandishi kutoka Radio washirika wetu  Dar es salaam Tanzania Benedict Komba katika makala hii