Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNDP yuko Afrika ya Kusini kuchagiza malengo ya milenia

Mkuu wa UNDP yuko Afrika ya Kusini kuchagiza malengo ya milenia

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP Helen Clark amewasili nchini Afrika ya Kusini kwa ziara ya siku tatu kupigia upatu malengo ya milenia.

Akiwa nchini humo atakutana na Rais Jacob Zuma na viongozi wengine wa serikali na utakuwa na mjadala wa masuala ya kijinsia utakaoshirikisha viongozi wanawake kutoka katika Nyanja ya siasa, biashara, taaluma na habari. Bi Clark pia atazindua wimbo maalumu wa Umoja wa Mataifa wa malengo ya milenia kwa ajili ya mashindano ya kombe la dunia la kandanda litakalofanyika nchini humo mwaka huu wa 2010.

Wimbo huo utaimbwa na wanmuziki wanane mashuhuri wa Afrika akiwemo Yvonne Chaka Chaka, Angelique Kidjo na Oliver Mtukudzi.

(CLIP SONG)

Wimbo huo unachagiza jitihada za kufikia malengo manane ya milenia na sehemu ya kampeni ya kimataifa inayofanywa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa viongozi wa dunia wa malengo ya milenia utakaofanyika mwezi septemba New York. Bi Clark yuko Afrika ya Kusini kama sehemu ya ziara yake ya mataifa manne ya Afrika ambao ameshakwenda Mali, Burkina Faso na Tanzania.