Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imetahadharisha juu ya kuendelea kuzorota kwa hali nchini Somalia

UNHCR imetahadharisha juu ya kuendelea kuzorota kwa hali nchini Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa tahadhari juu ya hali inayoendelea kuzorota kwa kasi nchini Somalia na ongezeko la wakimbizi wa ndani.

Shirika hilo sasa linaomba fedha za ziada ili kuwasaidia wakimbizi wa Kisomali walioko katika nchi jirani za Kenya, Yemen, Ethiopia na Djibout, pamoja na wakimbizi wa ndani walioko katika maeneo mbalimbali ya Somalia. Maombi hayo ya msaada yametolewa leo mjini Geneva kwa lengo la kuwasaidia wakimbizi na pia kupanua kambi ya wakimbizi ya Ifo eneo la Daadab kwenye mkoa wa Kaskazini nchini Kenya.

Fedha zilizoombwa leo ni dola milioni 60 ingawa bajeti ya UNHCR mwaka huu ni dola milioni 424.7. Hadi sasa UNHCR imeshapokea asilimia 36 ya mahitaji ya bajeti yake. Alexander Alainikoff ni naibu kamishina mkuu wa UNHCR anaelezea changamoto inayowakabili Somalia.