Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNAMID amesema wanajeshi watajitetea endapo watashambuliwa

Mkuu wa UNAMID amesema wanajeshi watajitetea endapo watashambuliwa

Mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID amesema wanajeshi hao watajibiza mashambulizi yatakayofanywa dhidi yao.

Bwana Ibrahim Gambari amesema kikosi hicho cha pamoja kilipelekwa Darfur mwezi Januari mwaka 2008 na kufikia sasa UNAMID imeshapoteza walinda amani 24 baada ya kushambuliwa.

Katika mkutano wa pande tatu ulioamaliza mjini Addis Ababa jana serikali ya Sudan kwa mara nyingine imeahidi kuchukua hatua zote ili kuhakikisha usalama wa UNAMID. Gambari hata hivyo amesisitiza kuwa usitishwaji mapigano ni suluhu muhimu