WFP imetunukia tuzo Rais wa Brazili kwa jitihada zake za kupambana na njaa

10 Mei 2010

Shirika la Mpango wa chakula Duniani ( WFP) limemtunukia Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva tuzo ya kuwa kinara wa kimataifa katika vita dhidi ya njaa.

Tuzo hiyo amekabidhiwa kiongozi huyo wa Brazil na mkuu wa WFP Josette Sheeran wakati wa ziara yake rasmi nchini Brazil ambayo imekamilika leo jumatatu.

Bi Sheeren amesema shirika lake na serikali ya Brazil wana malengo sawa ya azimio la kuwa na dunia isio na njaa na kuongeza kuwa Rais Lula ameonyesha uongozi katika jitihada yake ya kutoa kipaumbele katika mahitaji ya watu masikini katika jamii na watu wasiokuwa na chakula cha kutosha, katika nyanja ya kimataifa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter