Wakimbizi wa DRC wailalamikia UNHCR nchini Burundi ili iwasaidie

7 Mei 2010

Maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hususani maeneo ya mashariki wako nchini Burundi.

Wakimbizi hao waliotoroka mapigano baina ya majeshi ya serikali na makundi ya waasi wanasema wanapata adha nchini Burundi hasa wale ambao hawana vibali rasmi vya ukimbizi. Wanliomba shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kusikiliza kilio chao na kuwafuta machozi.

Mwandishi wetu wa eneo la Maziwa Makuu Ramadhan Kibuga amekwenda kuonana na wakimbizi hao ambao waliokuwa wamepiga kambi nje ya ofisi za UNHCR nchini Burundi kutaka msaada .Ungana naye katika makala hii

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter