Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya afrika amekwenda Tanzania

Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya afrika amekwenda Tanzania

Mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhsu masuala ya Afrika Cheick Sidi Diarra leo ameelekea , Arusha Tanzania kuhudhuria mkutano wa siku mbili.

Mkutano huo utakaoanza Jumapili unahusu msaada wa Japan wa maendeleo barani Afrika.

Mkutano huo uthudhuriwa na mawaziri kutoka barani Afrika na wawakilishi wa serikali ya Japan na pia sekta binafsi ili kutathimini mpango uliopitishwa Yokohama mwaka 2008 kuchagiza maendeleo barani Afrika.

Bwana Diarra anasema Japan ilidhatiti kuongeza mara mbili msaada wake rasmi wa maendeleo Afrika ifikapo 2012 na pia kuongeza mara mbili kiwango cha uwekezaji wa makampuni binafsi. Ameongeza kuwa serikali ya Japan imeweka mfumo wa kushawishi wawekezaji kuwekeza barani Afrika.