Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran kupata fursa kuthibitisha nia yake ya nyuklia kwenye mkutano katika UM

Iran kupata fursa kuthibitisha nia yake ya nyuklia kwenye mkutano katika UM

Kongamano la kimataifa litafanya kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wiki ijayo. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kongamano hilo Iran itapata fursa kuhakikishia ulimwengu kuhusu mipango yake ya nyuklia kuwa ni ya amani.

Mwenyekiti huyo pia amezitaka nchini wanachama kubadilishana mawazo ya jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia duniani.

Rais wa sasa wa mkataba wa kupinga uzalishaji wa nyuklia NTP ambaye ni balozi Libran n Cabactulan wa Ufilipino amewaambia waandishi wa habari mkutano huo unatoa nafasi ya kutathimini nini kinawezekana katika upunguzaji wa silaha za nyuklia na pia matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia.