Ban ameitaka jumuiya ya kimataifa kuinga mkono mahakama ya ICC
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyataka mataifa yote kuiunga mkono mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoko The Hague Uholanzi.
Katika semina maalumu kuhusu mahakama hiyo iliyo iliyoitwa tathimini ya changamoto za mahakama ya ICC, Ban amesema mahakama hiyo ni kiungo muhimu cha mfumo wetu wa kimataifa wa haki. Amesema ni mara moja tuu kila nchi iliridhia mkataba wa Roma na kuchukua hatua muhimu kuhakikisha mkataba huo unafanya kazi hata katika ngazi ya taifa, hasa kuhakikisha wanaotenda uhalifu hawapewi mwanya wa kukwepa mkono wa sheria.
Hata hivyo kwa kuwa pia sio nchi zote zilizoridhia mkataba wa Roma Ban amesema hiyo ndio changamoto kubwa inayoikabili mahakama ya ICC.