Skip to main content

Zaidi ya Warundi laki moja wajivunia kuwa raia wapya wa Tanzania

Zaidi ya Warundi laki moja wajivunia kuwa raia wapya wa Tanzania

Hatua ya hivi karibuni ya serikali ya Tanzania kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi zaidi ya laki moja na sitini kimepongezwa kimataifa.

Hatua hiyo imefikiwa kwa ushirikiano mkubwa wa serikali ya Burundi na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.Tanzania ambaye imekuwa mhifadhi wa maelfu ya wakimbizi kutoka Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi inajulikana kama kisiwa cha amani.

Sasa nchi hiyo imeamua kuwapa hadhi ya uraia wakimbizi hao ambao wengu wamekuwepo nchini humo kwa zaidi ya miaka 30. Burundi kwenyewe hatua hiyo imepokelewa kwa nderemo na vifijo kama alivyobaini mwandishi wetu mjini Bujumbura Ramadhan Kibuga.