Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wa mtaa wa mabanda Kenya wawafariji wenzao wa Haiti kwa wimbo

Watoto wa mtaa wa mabanda Kenya wawafariji wenzao wa Haiti kwa wimbo

Kundi la muziki lijulikanalo kama Wafalme linalojumuisha watoto wa mitaa ya mabanda Kenya limeamua kuwafariji watoto wenzao wa Haiti kwa njia ya wimbo baada ya athari za tetemeko na kipindupindu.

Watoto hao wa kundi la  Wafalme, wameguswa sana na athari zinazowakabili maelfu ya watoto wa Haiti ambao kwa sasa wanakabiliwa na wakati mgumu kwa sababu ya tetemeko la ardhi la 12 Januari 2010 na kipindupindu ambacho kinaendelea kuisumbua nchi hiyo.

Kundi la Wafalme wamefadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, la mazingira UNEP na na la makazi UN-HABITAT na wametoa kanda ya video ya wimbo unaochagiza amani, upendo na umoja.

Kwa nini watoto hawa wa mtaa wa mabada wakaamua kuwafariji wenzao wa Haiti kwa njia ya wimbo? Jason Nyakundi mjini Nairobi amewatafuta watoto hao na kunena nao. Ungana naye kwenye makala hii

(PKG BY JASON NYAKUNDI)