Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa leo kutoa ripoti ya kuhusu mauaji ya Benazir Bhutto

Umoja wa Mataifa leo kutoa ripoti ya kuhusu mauaji ya Benazir Bhutto

Umoja wa Mataifa leo unatazamiwa kutoa ripoti baada ya uchunguzi wa mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan Benazir Bhutto.

Ripoti hiyo inatolewa baada ya tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa kutafuta ukweli wa mauaji hayo ya mwaka 2007 kukamilisha uchunguzi.

Awali ripoti hiyo ilikuwa itolewe Machi 31 lakini ikaahirishwa hadi leo Aprili 15 kutokana na ombi maalumu la Rais wa Pakistan Asif Alli Zardari ambaye alikuwa mume wa Bhutto.

Tume hiyo ya uchunguzi ilianza kazi yake Julai mwaka 2009 baada ya Pakistan kuomba ifanye hivyo.Tume hiyo itakabidhi ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Tume hiyo ilikuwa na wajumbe watatu, ikiongozwa na Balozi wa Chile Heraldo Mupoz, na wengine ni Marzuki Darusman mwanasheria mkuu wa zamani wa Indonesia na Peter Fitzgerald mkongwe katika jeshi la taifa la Ireland ambaye pia ameshafanya kazi na Umoja wa Mataifa katika Nyanja mbalimbali.