Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya Moghadishu Somalia

WHO imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya Moghadishu Somalia

Nchini Somalia licha ya matatizo ya kiusalama shirika la afya duniani WHO limefanikiwa kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya mjini Moghadishu.

Mafunzo hayo yamewahusisha madaktari 33, wauguzi na wakunga, yakiwa na lengo la kuimarisha ujuzi wao hususani katika kukabiliana na ongezeko la machafuko mjini humo.

WHO ilimtuma daktari mtaalamu wa athari za vita ili kutoa mafunzo hayo kwa madaktari, wauguzi na wakunga yatakayowasaidia kuwatibu na kuwahudumia waathirika wa machafuko na pia kuwazalisha kina mama wajawazito.