Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yachagiza upimaji wa hiyari wa virusi vya HIV nchini Zambia

UNICEF yachagiza upimaji wa hiyari wa virusi vya HIV nchini Zambia

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudia watoto UNICEF amesema kuongeza upimaji wa hiyari wa virusi vya HIV na elimu kwa umma kutasaidia kukabiliana na ukimwi nchini Zambia.

Bi Ann M Veneman ameyasema hayo alipozuru nchini Zambia akitokea Lesotho. Zambia ni miongoni mwa nchi za Kusini mwa Afrika zilizoathirika sana na ukimwi. Zaidi ya Wazambia milioni moja inakadiriwa wamefariki dunia kwa ugonjwa wa ukimwi tangu miaka ya 1980.

Na Bi Veneman ametumia ziara yake nchini humo kusisitiza elimu kwa umma na kuchagiza watu kupima virusi kwa hiyari jambo ambalo amesema litasaidia katika vita dhidi ya ukimwi.