Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inatathimini ilivyokabiliana na mlipuko wa homa ya mafua ya H1N1

WHO inatathimini ilivyokabiliana na mlipuko wa homa ya mafua ya H1N1

Shirika la afya duniani WHO limeanza tathimini binafsi ya jinsi lilivyokabiliana na mlipuko wa homa ya mafua ya H1N1.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dr Margaret Chan amesema shirika hilo litasaidia kuwezesha tathimini ambayo ni binafsi, inayostahili na iliyowazi.

Homa ya mafua ya H1N1 imekuwepo kwa karibu mwaka mmoja sasa, na imesambaa karibu dunia nzima na kukatikli maisha ya watu wapatao 17,700. WHO imekuwa ikikosolewa vikali kwa jinsi ilivyokabiliana na mlipuko wa homa hiyo pamoja na utengenezaji wa chanjo.