Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ahofia hali ya wakimbizi wa Sahara Magharibi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ahofia hali ya wakimbizi wa Sahara Magharibi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea ongezeko la hofu yake juu ya haki za binadamu katika mgogoro wa Sahara Magharibi.

Koloni hilo la zamani la Hispania liko katika mgogoro na Morocco ambayo inadhibiti eneo kubwa na POLISARIO Front chama kinachotaka uhuru wa eneo hilo. Mkataba wa kusitisha mapigano ulimaliza vita dhidi ya Morocco na POLISARIO Front mwaka 1991. Kura ya maoni ilitarajiwa kupigwa mwaka 1992 ili kuwaruhusu watu wa eneo hilo kuamua kati ya kujitenga na kuwa huru au kuunganishwa na Morocco, lakini hadi leo kura hiyo haijapigwa.

Katika ripoti yake ya karibuni ya mpango wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kura ya maoni Sahara ya Magharibi MINURSO, Katibu Mkuu amesema kumekuwepo na mikutano miwili isiyo rasmi mwaka jana na mwaka huu ili kujaribu kutatua mzozo huo lakini haiajazaa matunda. Amesema kazi ya ziada inahitajika kabla ya duru nyingine ya majadiliano ambayo ni rasmi kuweza kufanyika.