Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan inatarajia kupiga kura jumapili lakini kuna hofu juu ya nia na uhalali wa uchaguzi huo

Sudan inatarajia kupiga kura jumapili lakini kuna hofu juu ya nia na uhalali wa uchaguzi huo

Ikiwa imesalia siku moja tuu kabla ya Jumapili wananchi wa Sudan kupiga kura, kuna hofu juu ya nia na uhalali wa uchaguzi huo. Bado kuna mkanganyo kuhusu ushiriki na kususia kwa vyama vya upinzani.

Taarifa ya mwakilishi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice kuhusu hofu ya serikali ya Obama kutokana na mambo yanayoendelea Sudan imekuwa ikiripotiwa. Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter yuko mjini Khartoum kwani shirika lake Carter Center linajiandaa kuwa miongoni mwa waandalizi wa uchaguzi huo.

Hata hivyo kwa upande wake mgombea Urais wa chama tawala ambaye ni Rais wa sasa Hassan Al-Bashir aliyetolewa kibali cha kumatwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ameahidi kwamba uchaguzi huo wa mwishoni mwa wiki hautokuwa tu huru na wa haki, bali pia utakuwa msafi na mfano wa kuigwa.