Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo anashiriki kikao cha bodi ya wakurugenzi wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo anashiriki kikao cha bodi ya wakurugenzi wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon bado yuko Vienna Austria katika ziara itakayokamilika kesho.

Ban akiwa nchini humo amekutana na viongozi wa serikali na wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la vikosi vya kulinda amani, Afghanistan na Mashariki ya Kati.

Leo Bwana Ban anahudhuria mkutano wa bodi ya wakurugenzi wa Umoja wa Mataifa na pia atahutubia baraza la kudumu la shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE.