Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa Kisomali wanaovuka Ghuba ya Aden imepungua licha ya machafuko

Idadi ya wakimbizi wa Kisomali wanaovuka Ghuba ya Aden imepungua licha ya machafuko

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema idadi ya watu wanaovuka Ghuba ya Aden na bahari ya shamu kutoka pembe ya Afrika imepungua licha ya machafuko yanayoendelea Somalia.

UNHCR inasema kuanzia mwanzo wa mwaka huu zaidi ya watu 9,000 wamewasili mwambao wa Yemen tofauti na idadi ya karibu watu 17,000 walioingia mwaka jana 2009 kati ya mwezi Januari na Machi. Na idadi kubwa ya watu waliopungua imesemekana kuwa ni Wasomali. Takribani Wasomali elfu tatu tu ndio walioingia Yemen mwaka huu ambao ni theluthi tu ya walioingia robo ya kwanza ya mwaka jana.

Msemaji wa UNHCR Melisa Fleming anasema kupungua huko kwa Wasomali wanaoingia Yemen sio kutokana kuimarika kwa hali ya mambo Somalia.