Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unasema uko Afghanistan kwa ajili ya kusaidia sio kutawala

UM unasema uko Afghanistan kwa ajili ya kusaidia sio kutawala

Mwakilsi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Staffan de Mistura amesema watu wa Afghanistan wameteseka kiasi cha kutosha katika miongo miwili iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kabul Mistura ameelezea umuhimu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupisha azimio la kuongeza muda wa mpango wake wa kulinda amani Afghanistan UNAMA.

Pia amesema UNAMA ipo nchini humo kwa ajili ya kusaidia na sio kuongoza. Amenukuliwa akiunga mkono mazungumzo ya amani baiana ya serikali ya Afghanistan na kundi kubwa na wanamgambo linalohusiana na Taliban