Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tovuti kutumika katika kampeni ya kupambana na malaria

Tovuti kutumika katika kampeni ya kupambana na malaria

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria leo amezindua kundi jipya la watumiaji wa tovuti ,kuchagiza na kushirikisha vyombo vya habari na wasikilizaji,watazamaji na wasomaji wao katika vita dhidi ya malaria.

Mwakilishi huyo Ray Chambers amesema kundi hilo litatumia uwezo wake kuwafikia wafuasi wao kwenye tovuti na wasiotumia tovuti katika mchakato huo, kuwaelezea pia athari, njia za kujikinga na mambo yanayohitajika ili kufikia malengo ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kuzipa uwezo nchi zote zenye tatizo la malaria kuzuia ugonjwa huo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2010.

Shirika la afya duniani Who linasema watu takribani bilioni 3.3 ambayo ni karibu nusu  ya watu wote duniani wako katika hatari ya kuugua malaria. Kila mwaka watu milioni 250 wanaugua malaria na karibu watu milioni moja hufa kutokana na ugonjwa huo.