Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

serikali ya Junta Myanmar bado inakiuka haki za binadamu

serikali ya Junta Myanmar bado inakiuka haki za binadamu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Myanmar Tomas Ojea Quintana ameongeza shinikizo dhini ya serikali ya Junta ya Myanmar.

Bwana Quintana akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva, ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kabla ya uchaguzi mkuu wan chi hiyo ili kubaini endapo serikali hiyo ya Junta ina hatia ya uhalifu wa vita na ukatili dhidi ya ubinadamu.

Serikali ya Myanmar imekuwa ikilaumiwa kwa kukiuka haki za binadamu hasa kwa kuwashikilia wanasiasa wa upinzani bila kuzingatia misingi ya sheria akiwemo Aung San Suu Kyii.