Jamhuri ya Korea yanyooshewa kidole kuhusu haki za binadamu

Jamhuri ya Korea yanyooshewa kidole kuhusu haki za binadamu

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu imeisonta kidole Jamuhuri ya watu wa Korea kwa ukiukaji wa haki.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini humo Profesa Vitit Muntarbhorn.

Akizungumzia kuhusu ripoti hiyo mbele ya waandaishi wa habari mjini Geneva, profesa Muntarbhorn amesema ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu imebaini kuwa Jamuhuri ya watu wa Korea inakiuka haki hizo katika nyanja mbalimbali.