Matokeo ya awali yaashiria mchuano mkali nchini Iraq
Kwa mujibu wa matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge yaliyotolewa leo nchini Iraq, waziri mkuu Nour al-Maliki anaonekana kuwa mbele kwa kura chache dhidi ya mpinzani wake wa Kishia.
Ingawa Wasuni wengi walijitokeza katika uchaguzi wa Jumapili iliyopita safari hii tofauti na mwaka 2005, ambapo ghasia na mgomo uliwafanya wasipige kura, wengi bado wana hofu kama kweli kutakuwa na mabadiliko yoyote ya kuwapa nafasi ya kukidhi haja yao ya madaraka.