Ghasia zachelewesha kampeni ya chanjo Nigeria

Ghasia zachelewesha kampeni ya chanjo Nigeria

Kampeni ya chanjo ya polio katika jimbo la Jos lililoghubikwa na ghasia katikati mwa Nigeria itachelewa kuanza.

Kampeni hiyo sasa itaanza Machi 13 ambapo mbali ya ghasia pia wafanyakazi wa afya wako katika mgomo. Chris Maher mkuu wa operesheni za kutokomeza polio wa Umoja wa Mataifa nchini humo anasema kuendesha shughuli za chanjo katika eneo hilo lenye ghasia ni changamoto na ni hatari kwa wafanyakazi.

Mipango ya WHO ni kubadilisha muda ili chanjo hiyo iweze kuwafikia watoto wengi zaidi huku pia ikiwalinda wafanyakazi wake.