Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lajadili haki za watoto

Baraza la haki za binadamu lajadili haki za watoto

Baraza la haki za binadamu leo limeanza mkutano wake wa kila mwaka kuhusu haki za mtoto na ukatili wanaotendewa.

Mwaka huu kauli mbiu ni vita dhidi ya ukatili wa kimapenzi kwa watoto, ukijadili mbinu za kuzuia ulawiti kwa wavulana na wasichana. Mkutano huo umesema miongoni mwa vitu vinavyochangia watoto kuwa katika hatari ya kulawitiwa ni mfumo wa magereza katika nchi nyingi ambao huwafunga watoto na watu wazima pamoja.

Kwa mujibu wa mkutano huo idadi ya watoto wanaofungwa inaongezeka. Manfred Nowak ni mwakilishi maalumu kuhusu masuala ya utesaji.