WHO inawasaidia walioathirika na maporomoko nchini Uganda
Mpango wa kimataifa wa dharura wa afya HAC umeidhinisha dola elfu 50 kwa shirika la afya duniani WHO nchini Uganda ili kusaidia mahitaji ya madawa na matibabu kwa walioathirika na maporomoko ya ardhi yaliyoanza tarehe 25 Februari.
Zaidi ya watu laki 3 kwenye maeneo ya mlima Elgon, Butaleja, Budaka na Tororo wameachwa bila makazi na maporomoko hayo na vyanzo vya maji na vyoo vimeharibiwa na hivyo kutoa tishio la kuripuka magonjwa ya kuambukiza.
Watu 104 wamearifiwa kushikwa na ugonjwa wa kuhara na serikali ya Uganda inaongoza shughuli za masuala ya afya kwa kushirikiana na WHO kama anavyofafanua afisa wa WHO.