Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wahofia kuzuka magonjwa baada ya mafuriko nchini Kenya

UM wahofia kuzuka magonjwa baada ya mafuriko nchini Kenya

Shirika ya Umoja wa Mataifa linalohusika na kuratibu masauala ya kibinadamu OCHA linasema maeneo ya Kenya yaliyofurika hivi karibuni huenda yakakumbwa na magonjwa ya kuambukiza yatokanayo na maji.

Msimu wa mvua nchini Kenya ambao ndio kwanza umeanza na unatarajiwa kuendelea hadi mwezi Juni, umeshaua watu 11 na kuwaathiri wengine 8,300 katika mikoa ya kaskazini, kaskazini mashariki na magharibi.

OCHA inasema mamia ya mifugo yamesombwa na mafuriko na mashamba kuharibiwa vibaya hasa katika maeneo ya mpakani na Uganda ambako maporomoko ya udongo yamewafanya maelfu kuzikimbia nyumba zao.

Katika wilaya ya Kati ya Isiolo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limegawa clorine kwa ajili ya watu kusafisha maji ya kunywa.