Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya nusu ya walioathirika na tetemeko Haiti wamepata malazi

Zaidi ya nusu ya walioathirika na tetemeko Haiti wamepata malazi

Ikiwa ni chini ya miezi miwili tangu tetemeko kubwa kulitikisha eneo la kusini mwa Haiti na kuwaacha watu wapatao milioni 1.3 bila makazi, mashirika ya misaada ya kibinadamu yanayogawa vifaa kwa ajili ya malazi yanasema yamewafikia watu 650,000 ambao ni zaidi ya nusu ya waathirika.

Maelfu kwa maelfu ya vifaa kama mahema, kamba, na mbao vinaendelea kumiminika kisiwani Haiti ili kuwasaidia kupata malazi maelfu ya watu kabla ya msimu wa mvua utakaoanza mwezi May.

Hii ni hatua kubwa amesema Gregg McDonald ambaye anaongoza timu ya wataalamu wa kuratibu masuala ya malazi Haiti, chini ya ofisi ya shirikisho la kimataifa la msalaba mwekundu na mwezi mwekundu.