Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Inawezekana kutokomeza maambukizi ya HIV kwenda kwa mtoto

Inawezekana kutokomeza maambukizi ya HIV kwenda kwa mtoto

Lengo la kutokomeza mambukizi ya virusi vya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ifikapo mwaka 2015 ni jambo linalowezekana.

Hata hivyo imeelezwa kwamba itawezekana tuu endapo hatua za sasa zilizofikiwa na programu zinazofadhiliwa na mfuko wa kimataifa na juhudi zingine zitaendelezwa. Malaria huenda ikamalizwa kabisa kama tatizo la kiafya la umma ndani ya muongo mmoja katika nchi ambazo ugonjwa huo ni sugu.

Kifua kikuu katika nchi nyingi sasa kimeanza kupungua na lengo la kimataifa la kupunguza nusu ya matatizo ya kifua kikuu ifikapo 2015 linaweza kufikiwa. Huu ni utabiri wa ripoti ya mfuko wa kimataifa ya mwaka 2010 iliyotolewa leo. Profesa Rifat Atun ni mkurugenzi wa mipango na utendaji

wa mfuko wa kimataifa