Skip to main content

Ban ki-moon ahitimisha ziara Chile na kuahidi msaada

Ban ki-moon ahitimisha ziara Chile na kuahidi msaada

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehitimisha ziara yake katika maeneo yaliyoathirika nchini Chile, kwa ahadi ya kuisaidia nchi hiyo katika juhudi za kurejea katika maisha ya kawaida baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi.

Bwana Ban ameahidi msaada wa dola milioni 10 ambazo zitatolewa mara moja na Umoja wa Mataifa. Ban alitembelea eneo la Concepcion ambako madaktari wameonya kuzuka kwa magonjwa na athari zingine za afya kutokana na kifusi na ukosefu wa maji safi.

Wakati akiondoka bwana Ban amewaambia watu wa Chile kumbukeni tuko pamoja nanyi, sala na mioyo yetu iko pamoja nanyi, hako peke yenu.