Watu zaidi ya 30 wameuawa nchini Iraq katika shambulio la kujitoa mhanga

Watu zaidi ya 30 wameuawa nchini Iraq katika shambulio la kujitoa mhanga

Mashambulizi yaliyofuatana ya kujitoa muhanga katikati ya mji wa Bauba nchini Iraq leo, yamewaua watu 33 na kujeruhi wengine 55. Mashambulizi haya yamefanyika siku chache tuu kabla ya taifa zima kupiga kura ya uchaguzi wa bunge utakaofanyika mwishoni mwa wiki.

Shambulio hilo ambalo ni baya zaidi kuikumba Iraq katika kipindi cha mwezi mmoja limewafanya polisi mara moja kutangaza hali ya kutotembea hovyo katika mji huo mkubwa kuliko yote nchini Iraq .

Karibu askari na polisi milioni moja wameweka katika hali ya tahadhari kuelekea uchaguzi huo wa Jumapili ambao watu wnahofia huenda ukairejesha nchi hiyo katika machafuko ya kidini.