Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua mpango wa miaka 5 kuwasaidia wanawake kupambana na Ukimwi

UM umezindua mpango wa miaka 5 kuwasaidia wanawake kupambana na Ukimwi

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS kwa kushirikiana na msanii na mwanaharakati wa masuala ya wanawake na ukimwi Annie Lenox wamezindua mpango waliouita "Ajenda ya kuzichagiza nchi kuchukua hatua kwa ajili ya wanawake, wasichana, usawa wa kijinsia na HIV mwaka 2010 hadi 2014".

Ajenda hiyo ni kwa ajili ya kushughulikia dosari katika usawa wa kijinsia, na ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea kuwaweka wanawake na wasichana katika hatari ya kuambukizwa virusi vya ukimwi.

Mpango huo umezinduliwa katika kikao cha 54 kinachojadili hali ya wanawake katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York