Urusi yatoa wito wa suluhu ya kidiplomasia dhidi ya mipango ya nyukilia ya Iran

Urusi yatoa wito wa suluhu ya kidiplomasia dhidi ya mipango ya nyukilia ya Iran

Serikali ya Urusi imesema ni lazima kutafuta suluhu ya kidiplomasia kutatua masuala ya nyuklia ya Iran na cha muhimu ni kutatua mzozo huo kwa njia ya amani.

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin amewaambia waandishi wa habari kwamba ni lazima kupata suluhisho na ikiwezekana kuwa na majadiliano na Iran. Ameongeza kuwa itakuwa bora kwa Iran kuweka msimamo utakaofungua njia ya majadiliano kwani itasaidia kuwa na mazungumzo yatakayozaa matunda.

Marekani inausukuma Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vipya dhidi ya Itan ikihofia kwamba Tehran inaunda silaha za nyuklia. Lakini Iran imeendelea kusisitiza kwamba mipango yake ya nyuklia ni ya amani.