Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano mkubwa wa masuala ya Darfur wafanyika Rwanda

Mkutano mkubwa wa masuala ya Darfur wafanyika Rwanda

Leo mkutano mkubwa wa masuala ya Darfur unaosimamiwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan unafanyika mjini Kigali Rwanda.

Mkutano huo unalengo la kuweka msimamo wa pamoja wa jinsi ya kusonga mbele katika kurejesha amani ya kudumu Sudan na hususani kwenye jimbo la Darfur.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigali mwakilishi huyo Professa Ibrahim Gambari amewaambia waandishi wa habari amefurahi Rwanda kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo. Amesema ni muhimu watu wenye majukumu kwa Darfur kukutana pamoja ili kujadili na mwakilishi wan nchi wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na kuona njia gani ya kuifuata ili kurejesha amani ya kudumu Darfur. Bwana Gambari ameambatana na kamanda wa vikosi vya UNAMID ambaye anatoka nchini Rwanda Luten Jenerali Patrick Nyamvumba.