Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa watoto lazima upewe kipaumbele kwenye amani ya Afghanistan

Ulinzi wa watoto lazima upewe kipaumbele kwenye amani ya Afghanistan

Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na migogoro ya kutumia silaha Radhika Coomaraswamy katika kuhitimisha ziara yake ya siku sana nchini Afghanistan amesema kuwalinda watoto lazime kuwe ndio kitovu cha ajenda ya mapatano kama ilivyoidhinishwa na jamii ya kimataifa.

Amesema wakati kuna uwezekano wa amani katika bunge la nchi hiyo Jirga na kufanyika mkutano mjini Kabul anataka kuhakikisha kwamba masuala ya watoto yanajumuishwa katika ajenda za matukio yoye hayo.

Coomaraswamy ameyasema hay oleo kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Kabul. Amesema anadhani serikali ya Afghanistan imeonyesha nia ya kisiasa ya kushughulikia masuala ya watoto na vita vya kutumia silaha. Imeunda kamati katika kiwango cha wizara ambayo itakuwa ikishirikiana na Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na mgogoro wa kutumia silaha.