Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya kifo ni ngumu na nyeti kwa jamii nyingi

Hukumu ya kifo ni ngumu na nyeti kwa jamii nyingi

Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amesema tusisahau ukweli kwamba kufuta hukumu ya kifo ni vigumu na ni mchakato nyeti kwa jamii nyingi.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa kongamano la nne la dunia linaopinga hukumu ya kifo. Amesema mwaka 2007 baraza la Umoja wa Mataifa liliridhia azimio namba 62/149 linalotoa wito kwa ncho zote ambazo bado zinatekeleza hukumu ya kifo kuandaa mikakati ya kufuta hukumu hiyo. Na anasema msimamo wa Umoja wa Mataifa hauajabadilika.