Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM na washirika wake waendelea kuisaidia Haiti

Mashirika ya UM na washirika wake waendelea kuisaidia Haiti

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu OCHA inasema idadi ya watu wanaoondoka mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince inaongezeka.

Inakadiriwa kuwa watu 160,000 wamehamia katika maeneo ya mpakani na Jamuhuri ya Dominican.Wengi wao ni watu walioachwa bila makazi na tetemekola ardhi na wamepokelewa na familia, hivyo wamefanya idadi ya watu katika familia moja kuongezeka kutoka watano hadi kumi.

Mashirika mengine kama UNICEF na WHO wanaendelea kutoa msaada unaohitajika wa maji, usafi , ujenzi wa vyoo na madawa. Nalo shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM linasema ,linaisaidia serikali ya Haiti kuwaandikisha wakimbizi wa ndani na kutambua wanakotoka.

Lengo ni kutatua tatizo la msongamano katika makazi ya muda mjini Port-au-Prince kama anavyoeleza Chris Lom wa IOM.