Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Irani kuongeza uzalishaji wa uranium kwa 20%

Irani kuongeza uzalishaji wa uranium kwa 20%

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amemtaka mkuu wa masuala ya nyuklia wa nchi hiyo kuanza uzalishaji wa Uranium hadi aslimia 20%.

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo kunamvutano baiana ya nchi hiyo na nchi za magharibi zikiitaka Iran ibadili uzalishaji wa uranium na kuwa na uzalishaji wa nishati ya nyuklia.

Taarifa zinasema maagizo ya Rais Ahmadinejad yalifuatiwa na tangazo la mkuu wa shirika la nishati ya atomic wa Iran ,kwamba leo Iran italiarifu shirika la kinmataifa la nguvu za atomic juu ya mipango yake itakayoanza kesho Jumanne kuzalisha uranium kwa asilimia hadi 20%.