Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen yaonya kuzuka matatizo baada ya wakimbizi kuongezeka

Yemen yaonya kuzuka matatizo baada ya wakimbizi kuongezeka

Wafanyakazi wa misaada na maafisa wa serikali nchini Yemen wameonya kutokea matatizo makubwa ya kibinadamu hasa ukosefu wa malazi na huduma muhimu kwa wakimbizi wa ndani nchini humo.

Hii imetokana na kuongezeka zaidi ya mara mbili ya wakimbizi hao na kufikia laki mbili na nusu tangu kuzuka kwa mapigano baiana ya jeshi la serkali na kundi linaloongozwa na waasi la Houthi 12 August mwaka jana.

Wafanyakazi wa misaada wanasema licha ya kuwepo na kambi tatu za wakimbizi wa ndani katika eneo la Hajjah , upungufu wa malazi ndio hofu yao. Wakimbizi wengi wa ndani nchini Yemen wanaishi katika mabanda yaliyoko kando mwa barabara kuelekea kwenye kambi za wakimbizi.